KARIBU KENYA RAISI WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN

KARIBU KENYA RAISI WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN

Karibu Raisi wa Tanzania hapa kwetu Kenya
Tulikungoja kwa hamu na gamu
Kwetu Kenya "Hakuna matata"
Pongezi Raisi shujaa Samia Suluhu Hassan

Juzi ulikua Uganda kwa safari ya kikazi
Na leo uko Kenya 
Kwa kweli Tanzania wamepata Raisi mchapa kazi
Pongezi Raisi shujaa Samia Suluhu Hassan

Ulipitisha juzi sheria za kunufaisha wananchi wa Tanzania
Leo uko Kenya kuunganisha biashara na maendeleo
Unapenda mapatano na uwiyano wa majirani
Pongezi Raisi shujaa Samia Suluhu Hassan

Wewe ni shujaa wa Tanzania na nchi zote za Africa mashariki
Nchi tatu za Africa mashariki hawajapata Raisi wa jinsia ya kike 
Raisi anapenda kuunganisha inchi za Africa mashariki wafanye kazi pamoja
Pongezi Raisi shujaa Samia Suluhu Hassan

Hapa Kenya tunakupenda kama "Sugar sukari"
Kwa sera na maadili Yako ya kusema na kutenda
Wewe ulichaguliwa na mungu na sisi pia twaja huko Tanzania ishallah
Pongezi Raisi shujaa Samia Suluhu Hassan

Tunakuomba uunge wanawake wengi wapate vyeo na nafasi za kazi za juu Tanzania
Kabla mwisho wa Mwaka, waite wanawake viongozi wa Africa mashariki kwa kongamano uwape siri za uongozi
Pongezi Raisi shujaa Samia Suluhu Hassan

Nakuombea heri njema na afya nzuri
Uongoze Tanzania kwa amani,upendo na umoja
Uwaletee heri na fanaka na maendeleo WaTanzania wainuke kimaisha.
Pongezi Raisi shujaa Samia Suluhu Hassan

Na
Veronica onjoro 
PhD student Mount Kenya University
onjoroveronica@yahoo.com

Comments

Popular posts from this blog

NI SABABU ZIPI ZINAZOFANYA MZUNGUMZAJI WA LUGHA KUFANYA MAKOSA YA KISARUFI NA KIMATAMSHI NA KIMANTIKI KATIKA LUGHA?

Methali, Vitendawili, nahau, misemo,

NADHARIA ZINAZOELEZEA CHIMBUKO LA FASIHI SIMULIZI/MASIMULIZI