Fafanua nadharia zozote tatu zitakazotumiwa na mwalimu wa sekondari kufunzia lugha ya pili.
1.
Fafanua
nadharia zozote tatu zitakazotumiwa na mwalimu wa sekondari kufunzia lugha ya
pili.
i.)
MBINU
YA USOMAJI.
Mbinu
hii inatumika kufundishia wanafunzi wanao jifunza lugha ya pili na ambapo
hawatarajiwi kutoka nje ya nchi ambapo
lugha hiyo inatumika. Lengo lake ni kuendeleza uwezo wa wanafunzi la kusoma
lugha ile. Vipengele vinavyofundishwa ni vile vya usomaji.
ii.)
NADHARI
YA MWALIMU ALIYE KIMYA.
Katika
mbinu hii, mwalimu anatakiwa kuwa kimyakwa muda mwingi darasani ilhali
mwanafunzi anatakikana kushirikishwa kuzungumza au kuandika kwa wingi.
Mbinu
hii imetengenezwa kwa misingi ifuatayo:
a)
Ujifunzaji
wa lugha ya pili unafanikishwa na vifaa halisi vya ufundishaji( vitu ambavyo
vanaweza kuonekana na kushikika)
b)
Kwamba
ujifunzaji wa lugha ya pili unafanikiwa ikiwa mwanafunzi anajigundulia mambo kwa
ubunifu wake badala ya kurudiarudia na kukumbuka anachojifunza.
c)
Ufunzaji
unafanikishwa kwa kushirikisha mwanafunzi kwa kile anachojifunza. Inashikilia
kwa wanafunzi ni watendaji na siyo wasikivu tu.
iii.)
NADHARIA
YA UFUNDISHAJI VITENDO
Nadharia
ya ufundishaji kwa vitendo hudhamiria kufundisha lugha kwa matumizi ya vitendo.
Wafuasi wa lugha hii huamini wanafunzi hujifunza lugha ya pili vizuri katika
mazingira na hali ambayo haina wasiwasi.
Husaidia
kuhitimisha wanafunzi wanaoweza
kuwasiliana bila vikwazo kwa sababu.
a.
Ufundishaji
wa lugha ya pili wapaswa kusisitiza maana na wala siyo miundo.
b.
Matumizi
ya vitendo amri ni muhimu katika ufundishaji wa lugha ya pili.
c.
Mwanafunzi
anaweza kujifunza vipande viwili vikubwa kuliko sentensi.
d.
Wanafunzi
husikiza na kujibu kwa vitendo.
e.
Usikilizaji
ukiimarika uzungumzaji huimarika pia.
2.
Eleza
umuhimu wa safu mbalimbali za ratiba
Ratiba ni orodha ya
mpangilio wa namna mambo yatakavyofuatana katika shughuli Fulani. Lengo lake ni
kuhakikisha wakati unatumiwa vizuri ili mambo Fulani yasije yakakosa kutendwa
kutokana na upungufu wa wakati.
Ratiba hutumiwa katika
mazishi, hafla, tamasha na kwa masomo.
Ratiba humwezesha
mwalimu kuhitimisha silabasi kwa muda uliopendekezwa.
Humwezesha mwalimu
kuamua namna
ya
kuhusisha mambo yanayohusiana na na kuamua mambo ya kusisitiza.
Humwezesha mwalimu
kupanga ufundishaji wake ili ulingane nan a ugumu wa mambo au ulingane na
kiwango cha lugha ya mwanafunzi na mpango wa mwalimu wa kutahini.
Ratiba humwezesha
mwalimu kufikiria na kuandaa vielezo na vifaa mwafaka.
Safu mbalimabali za
ratiba na umuhimu ufuatao.
-
Husaidia
kutaja shughuli yenyewe husika kwa mfano siku ya zawadi au somo
lenyewe.
-
Tarehe
husaidia kuonyesha ni lini shughuli
hiyo hufanyika.
-
Mahali
husaidia kueleza mahali ambapo shughuli hiyo itafanyikia kwa mfano katika
uwanja wa mchezo wa Tingolo au darasa
Fulani.
-
Muda
husaidia kuonyesha saa ambazo tukio limepangiwa kuanza na kukamilika.
-
Wahusika
husaidia kutaja watu waliopewa wajibu wa kutekeleza jambo Fulani kwa mfano
mwalimu huwa na shughuli za kutekeleza na wanafunzi pia huwa na shughuli
tofauti za kutekeleza.
-
Wiki
husaidia mwalimu kujua ni juma lipi la muhula na kutekeleza wajibu wake ili
kukamilisha kazi zake kwa wakati unaofaa.
-
Ratiba huwa na kupindi ambacho husaidia
mwalimu kujua anashughulikia kipindi kipi kwa juma hilo lililotajwa.
-
Maoni husaidia kufafanua jinsi shughuli
ilivyoendelea kama ilikuwa ya ufanisi au la.
Comments
Post a Comment