Fafanua nadharia zozote tatu zitakazotumiwa na mwalimu wa sekondari kufunzia lugha ya pili.
Fafanua nadharia zozote tatu zitakazotumiwa na
mwalimu wa sekondari kufunzia lugha ya pili.
Kunazo nadharia
(mikondo) za ufundishaji wa lugha ya pili
ambazo zimewahi kuathiri, na ambazo mpaka sasa zinaathiri, ufundishaji
wa lugha ya pili. Nadharia hizo ni nyingi.
a) Nadharia ya
ufundishaji wa moja kwa moja
Nadharia hii
ilitumika sana Ulaya mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.
Nadharia hii ilisisitiza sana ufundishaji wa lugha ya pili kwa kuitumia lugha
iyo hiyo. Iliwakataza walimu kutumia tafsiri ya aina yoyote katika ufundishaji
wao. Katika nadharia hii, ilikuwa ni marufuku kutumia lugha ya mama katika
ufundishaji wa lugha ya pili. Waasisi wa nadharia hii waliamini kuwa watu
wanaweza kujifunza lugha ya pili namna wanavyo jifunza lugha ya kwanza, pasi na
tafsiri au matumizi ya lugha nyingine yoyote. Kwao. Ujinzaji wa lugha ya pili
ulikuwa ni sawa na kuzifuata nyayo za lugha ya kwanza ambapo yule anayejifunza
huingiliana moja kwa moja na lugha anayojifunza bila tafsiri.
Nadharia ya
ufundishaji wa moja kwa moja haikuhimiza uchambuzi wa sarufi au maelezo ya
kisarufi kwa wanafunzi. Kwa mujibu wa nadharia hii, walimu walishauriwa
kutotaja maneno kama’Nomino’, ‘Kitenzi’ na ‘Kivumishi’. Baada ya ufundishaji
uliofanywa kwa uingizaji, na maonyesho ya vitu, kwa mfano, picha au vifaa
vingine, wanafunzi walitakiwa kuzing’amua wenyeye sheria na kanuni za kisarufi.
Wanadharia hii waliamini kuwa lugha hufunzika vizuri kwa kuitumia darasani na
wala siyo kuichambua kisarufi.
Kwa mujibu wa nadharia hii, walimu walitakiwa kufundisha mazungumzo pamoja na ufahamu wa kusikiza. Mbinu ya maswali na majibu ilipendekezwa katika ufundishaji wa mazungumzo ambayo yalithaminiwa sana. Mwalimu aliuliza maswali nao wanafunzi waliyajibu. Kadhalika katika uzungumzaji wanafunzi walitakiwa kujifunza matamshi bora yaliyo sawa ya wazawa wa lugha ya pili waliyokuwa wakijifunza.
b) Nadharia ya
utabia
Nadharia hii
ilitumika sana katika miaka ya hamsini (1950) hadi miaka ya sitini (1960) kule
Marekani. Baadhi ya vipengele vya nadharia hii vingali vinatumika mpaka leo.
Nadharia hii imejengwa katika misingi ya nadharia ya Saikolojia iitwayo Utabia.
Wafuasi wa
nadharia ya utabia walidhamiria kueleza namna tabia inavyojengwa. Waliamini
kuwa tabia itadumu ikiwa itaigwa, itarudiwarudiwa, na kutuzwa, lakini tabia
isiyorudiwa na isiyotuzwa hufifia.
Kwa hivyo
walisisitiza ujifunzaji wa lugha ni sawa na ujifunzaji wa tabia yoyote ile ya
binadamu,kama vile kuendesha baiskeli, kuogelea na kadhalika.Kwa hivyo
walipendekeza mambo yafuatayo katika ufundishaji wa lugha:
i) Kukariri na
kurudiarudia matamshi mazuri ya vipande vya mazungumzo , miundo ya
sentensi n.k
ii) Vipengele
vya lugha vifundishwe kwa njia ya kusikiliza na kuongea kwanza kabla ya
kuandikwa.
iii) Ufundishaji
wa sarufi na vipengele vingine vya lugha usifanywe kwa kuchambua vipengele vya
lugha. Mwanzoni wanafunzi wakariri na kurudia na kuiga vipengele hivyo kabla ya
kuvizoea.
iv) Jukumu la
mwanafunzi ni kufuata maagizo, ilhali lile la mwalimu ni kiongozi wa kila tukio
darasani
c) Nadharia ya mawasiliano
Nadharia ya
mawasiliano ilishika kasi na kupanuka nchini Uingereza katika miaka ya 1970.
Lengo kuu la nadharia hii ni kukuza uwezo wa kuwasiliana, lakini siyo kukuza
ujuzi wa miundo au vipengele vya lugha tu. Inakusudiwa kukidhi matakwa ya wale
wanaojifunza lugha ya pili katika mawasiliano. Mawasiliano yanahusu mambo mengi
kama vile, kusababisha mambo fulani yafanyike , kuboresha mahusiano kati ya
watu, na kuonyesha hisia za watu na ubunifu wao. Kadhalika, nadharia hii
inakusudiwa kuimarisha mbinu za ufundishaji ambazo zitasisitiza uhusiano uliopo
kati ya miundo ya lugha mawasiliano.
Nadharia ya
mawasiliano ina mihimili ifuatayo.
I. Maana ya miundo husisitizwa kwani
lengo kubwa la nadharia hii ni mawasiliano. Kwa mujibu wa nadharia hii,
madhumuni makuu ya lugha ni kuwasiliana, kwani lugha ni mfumo wa kueleza maana.
II. Vipashio muhimu vya lugha siyo vile
vya kisarufi na kimuundo tu, lakini pia vile vya kimawasiliano.
III. Malumbano (tamthilia fupi)
zilitumiwa kufundishia huwa hazikaririwi.
IV. Muktadha hupewa nafasi muhimu
katika ufundishaji. Kwa mfano, maneno mapya au miundo fulani ya kisarufi
huwekwa katika muktadha wa mawasiliano, kama vile katika sentensi, mazungumzo
na makala.
V. Drili zinafanywa lakini siyo za
lazima kwa mujibu wa nadharia hii
VI. Matamshi yanayoeleweka na watu
wengi katika mazungumzo ndiyo lengo kuu.
Lengo siyo matamshi yanayofanana na yale ya wazawa wa lugha.
VII. Kanuni za kisarufi na mbinu
nyinginezo zinatumiwa inapoonekana kuwa ni lazima.
VIII. Wanafunzi wanaweza kuzungumza
kuanzia siku ya kwanza.
IX. Lugha ya kwanza na tafsiri zinaweza
kutumiwa ikiwa hapana budi, pale matumizi yake yanaposaidia ufafanuzi wa jambo.
X. Kusoma na kuandika kunaweza kuanza
katika siku za mwanzo ikiwa ni muhimu.
XI. Matumizi ya lugha kwa wingi
darasani hupendekezwa kwani nadharia hii husisitiza kuwa mtu hujifunza lugha
vizuri kwa kuitumia
XII. Jukumu muhimu la ujifunzaji wa
lugha ni mawasiliano yanayofaa katika muktadha.
Nadharia ya
mawasiliano inapendekeza ufundishaji ambao unatumia shughuli zinazoedeleza
mawasiliano. Hii ni kwa sababu wafuasi wa nadharia hii wanaamini kuwa
ujifunzaji wa lugha huendelezwa na vitendo au shughuli zinazoendeleza
mawasiliano badala ya ukaririshaji wa miundo. Vitendo kama vile ulinganishaji
wa picha, maelezo yanayohusu ramani, maelezo ya ufanyaji wa shughuli fulani kwa
mfano, kupika chakula fulani, kuonyesha njia, mazungumzo ya vikundi, tamthilia
fupi, uingizaji, michezo, mijadala na usomaji wa magazeti hupendekezwa
darasani. Katika darasa la aina hii, mwalimu huchukuliwa kama mratibu wa
shughuli hiyo. Kazi yake muhimu huwa ni kuwezesha mawasiliano kuwapo kati ya
wanafunzi darasani. Mwalimu pia huwapa wanafunzi ushauri ufaao.
Ni vizuri kutaja
kwamba darasa linalotumia nadharia ya mawasiliano hushirikisha wanafunzi sana
katika mawasiliano. Mwalimu hasemi yote na kutenda yoye. Jukumu lake huwa
limebanwa kidogo. Wanafunzi huhimizwa kufanya mengi darasani.
Eleza umuhimu wa safu mbalimbali za ratiba.
Ratiba ya
kufundishia Kiswahili iko na safu mbalimbali. Safu hizo huwa na umuhimu mkubwa
kwa mwalimu wa Kiswahili. Zifuatazo ni safu za ratiba ya kufundishia Kiswahili
na umuhimu wake:-
(i)
Madhumuni ya muhula
Maazimio
ya kazi inafaa yatayarishwe kwa kuzingatia mfuatano wa mihula, kila muhula
ukiwa na maazimio yake. Kwa hivyo unapotayarisha kazi ya muhula ni lazima
uonyeshe maazimio yanayohusika ni ya muhula gani. Pamoja na hayo, kila muhula
inafaa ufafanue madhumuni ya ujumla ambayo unatarajia kutimiza katika muhula
unaohusika. Ni kutokana na madhumuni hayo ndipo baadaye unapoweza kupata
madhumuni maalum ya vipindi
(ii)
Mwezi
Kuhusu mwezi,
unachohitaji kutaja ni mwezi wa kufundishia. Kwa mfano, kama
ni muhula wa
kwanza, mwezi unaweza kuwa wa kwanza (Januari), wa pili (Februari), au
wa tatu (Machi).
(iii)
Juma / Wiki
Kwa sababu mwezi
wenyewe hugawanyika katika majuma/ wiki, inafaa
pia kuonyesha ni
wiki gani katika mwezi ambapo unapanga kufundisha jambo fulani
(iv)
Kipindi.
Ni vizuri pia
uonyeshe ni kipindi cha ngapi wiki hiyo. Kwa hivyo kabla ya kutayarisha
maazimio ya kazi
ni lazima uchunguze katika ratiba ya masomo ya shule ili ujue idadi ya
vipindi ambavyo
unatarajiwa kufundisha kila wiki katika somo lako. Kwa kawaida
vipindi vya
Kiswahili huwa ni vitano kila wiki lakini vinaweza vikawa vingi au vichache
zaidi kulingana
na mpango wa shule.
(v)
Mada / Yaliyomo
Mada ni kiini
cha somo au funzo muhimu katika kipindi fulani. Kwa mfano, mada
inaweza kuwa:
Insha ya methali. Kama hiyo ndiyo mada ya kipindi chako inakubidi pia
ujiulize kile
ambacho unatarajia wanafunzi wafanye kuhusu mada inayohusika. Tuseme,
kwa mfano,
kwamba unataka wanafunzi wako waandike insha inayobainisha ukweli wa
methali fulani.
Ni lazima ueleze jambo hili kwa kauli maalum; na unapofanya hivyo
utakuwa unatoa
lengo la kipindi.
(vi)
Madhumuni / Malengo ya
kipindi
Baada ya kuteua
mada ya kipindi ni lazima uteue kile ambacho unatarajia wanafunzi
wafanye kuhusu mada huska.Pamoja na kufafanua malengo / madhumuni maalum ya
kipindi ni lazima
upendekeze kazi
ya kushirikisha wanafunzi wakati kipindi cha somo kinapoendelea.
(vii)
Mazoezi / Kazi ya
wanafunzi
Kazi ya
kushirikisha wanafunzi ni lazima ihusiane na mada inayohusika pamoja na malengo
yaliyowekwa.
Kazi yenyewe inalenga kuchangia katika utekelezaji wa malengo
yaliyofafanuliwa.
Wakati mwingine kazi hii hujulikana kama enabling
objectives kwa
Kingereza. Ni
kupitia mazoezi haya / kazi hii ndipo malengo yanayotarajiwa kufikiwa
yanapoweza
kutimizwa.
(viii)
Vifaa / Marejeleo
Hali kadhalika,
unapotayarisha maazimio ya kazi unahitaji vifaa ambavyo huenda
ukavitumia
wakati wa kufundisha. Hivi navyo vimetengewa nafasi yake katika muundo
wa maazimio ya
kazi.
(ix) Maoni
Sehemu nyingine
muhimu ni ile ya maoni. Katika sehemu ya maoni unapaswa
kutoa maelezo
kuhusu jinsi mada fulani ilivyofundishwa. Unaeleza jambo lo lote ambalo
huenda lilitokea
na kuathiri utekelezaji wa mpango wako. Kila unapoandika maoni
kuhusu kipindi
cha somo huwa unajitathimini utendaji kazi wako. Maoni unayoandika
yanalenga
kukusaidia unapojiandaa kwa vipindi vitakavyofuata baadaye. Ikiwa kwa
mfano, kipindi
chako kilikuwa cha kufana, inafaa ueleze mambo ambayo yalichangia
kukifanikisha.
Hali kadhalika, ikiwa kipindi hakikufaulu kama ilivyotarajiwa inafaa
uonyeshe hatua
unazopanga kuchukua ili kurekebisha hali. Kwa hivyo, ni lazima utilie
maanani sana
mambo unayoandika kama maoni
Hata hivyo, kuna
aina nyengine yabratiba ambayo ni muhimu kuiangazia.
Ratiba ni orodha
ya mpangilio wa namna mambo yatakavyofuatana katika shughuli fulani. Lengo lake
ni kuhakikisha wakati unatumiwa vizuri ili mambo fulani yasije yakakosa
kutendwa kutokana na upungufu wa wakati.
Ratiba hutumika
katika sherehe, mikutano, mazishi, hafla, tamasha, n.k
Sehemu za Ratiba
Kichwa
Kichwa cha ratiba hutaja mambo yafuatayo:
Shughuli yenyewe – Taja jina la tukio
ambalo unaandalia ratiba. Kwa mfano Harusi ya Bwana na Bi Arusi, Siku ya Zawadi
Tarehe ya shughuli – je shughuli hiyo
itafanyika lini?
Mahali- Taja mahali ambapo shughuli
hiyo itafanyikia. kwa mfano katika uwanja wa michezo wa Kasarani, kanisa la St.
Mtakatifu
Mfano wa kichwa cha ratiba:
Ratiba ya Hafla ya Ukimwi katika
Bustani la Uhuru tarehe tano Januari.
Ratiba ya Mazishi ya Dkt. Marehemu
tarehe 20/12/1923 Kijijini Vikwazoni
Mwili
Mwili wa ratiba hujumuisha mambo mbalimbali
yatakayofanyika katika mpangilio maalum, saa mbalimbali. Ni vizuri kuzingatia
vipengele vifuatavyo:
Saa – Onyesha saa ambazo tukio
limepangiwa kuanza hadi linapotakiwa kumalizika
Mahali – Ikiwa shughuli tofauti
zinafanyika katika mahali mbalimbali kama vile vyumba tofauti, inapaswa hutaje
mahali ambapo kila jambo litafanyikia.
Wahusika – Taja mtu au watu waliopewa
wajibu wa kutekeleza jambo fulani. Hii huwasaidia kujitayarisha ipasavyo.
REFERENCE
Musau P.M. &
Chacha L.M. (2001): Mbinu sa Kisasa za Kufundisha Kiswahili,
Kenya Literature
Bureau.
5. Gerald Njagi
Matti (2002), Introduction to The Study of Literature, Institute of
Open Learning,
Kenyatta University.
6. K. W.
Wamitilia (2002), Uhakiki wa Fasihi Msingi na Vipengele Vyake. Phoenix
Publishers Ltd
Comments
Post a Comment