Hayakua ni maombi bali ulikua mchongoano

 Hayakua ni maombi bali ulikua mchongoano

Walikusanyika Kwa hoteli ya kifahari,
Wenye vyeo,mabwenyenye wa nchi ya Kenya,
Lengo lao tulidhani,maombi Kwa Rabuka,
Hasa maombi ya amani,ufisadi,upendo na umaskini,La hasha !
Hayakua ni maombi bali ulikua mchongoano

Nchi kila Kona ilitarajia maombi,
Lakini walivyosimama walikua ni wale wale,
Wa kawaida, tangatanga na kieleweke,
Jameni Mungu hafanyiwi dhihaka,
Hayakua ni maombi bali ulikua mchongoano

Maombi ya mwaka ujao twataka,
Yafanyiwe Uhuru park,na sote tualikwe,
Tutabeba chai zetu na vitoweo vyetu,
Hatutaki hoteli kubwa kubwa,maskini haingii,
Hayakua ni maombi bali ulikua mchongoano

Tamati nimefika huzuni umenipata,
Hata nyimbo zilikua za aibu jameni,
Mzaha mwaleta mbele ya maulana kwa nini hivi?
Kwa maombi duni yasiomridhisha Mungu,
Hayakua ni maombi bali ulikua mchongoano

Malenga kutoka Mombasa
Veronica onjoro
Mungu Ni mwema kila wakati

Comments

Popular posts from this blog

NI SABABU ZIPI ZINAZOFANYA MZUNGUMZAJI WA LUGHA KUFANYA MAKOSA YA KISARUFI NA KIMATAMSHI NA KIMANTIKI KATIKA LUGHA?

Methali, Vitendawili, nahau, misemo,

NADHARIA ZINAZOELEZEA CHIMBUKO LA FASIHI SIMULIZI/MASIMULIZI