JE,UPO UHUSIANO WA DHATI KATI YA KAMBUMBU NA MAHABA?

 


Je,upo uhusiano wa dhati kati ya kabumbu na 'Mahaba'?

'Kipendacho roho mara si moja huwa dawa na tabibu'. Kauli hii yafungua jamvi kwa.kufafanua paruwanja hali tata iliyowapata midomo achama wachezaji soka wawili. Wawili hawa walijipata tahanani taabani kwa kutuhumiwa tuhuma za ubakaji. Japo kwao kulikuwa sawa na kuku kumsingizia jogoo anapomkimbiza!
    Tuhuma hizo nzito mithili ya habta zenye nembo 'ubakaji' - haswa kwa wandani wao! Zilianza kumea matete kwa kasi.mno.Mmoja wa wachezaji hao ni Nguli Christiano Ronaldo huku mwenzake akiwa bingwa wa Paris- kijana machachari- Neymar.
    Wawili hawa kwa yakini,ni mabwanyeye wa haiba kama si wachezaji wenye uzito wa fulusi. Wanamiliki hela kuliko wanavyoitafuta. Hata si shani wala ajabu kwqo kuenda kupiga jiramba ugani kwa usafiri wa chopa za thamani isio na kadiri.
    Wanachokivuna kama mshahara kinadhihaki na kubeza ulimbo kuwa bidii hulipa. Kwani,malilioni ya mabunda ya pesa yanayoogelea kede kede kwao si mchezo wala machezo. Labda tukadirie hivi hivi tu.Walakini,tusienda chechele kwayo. Nisiwahadae kwa punje nusu. Nafahamu kuwa utamu wa chai sukari. 
      Hivi majuzi,kulingana na udukuzi na duru za hapa na pale,ripoti iliochipuka punde ni kwamba  jambia la sheria lililojinyoosha dede kumpiga chini tunu wa Juventus - Nyota - Christiano Ronaldo - limedondoka chini ghafula na kwa fajaa. Kuna ushahidi tosha na belele ya kuwa tuhuma za ubakaji uliozuka zilikiwa nunge na sufuri tu. Bali mshikemshike uliokuwapo ni 'hulka na silika za simba kuonja nyasi eti!'
    Kigoli aliyedaiwa kuwa kwenye kukurukakars zile alikiri kuwa alikuwa na hiyari yake wakati huo. Alisema;
''Baba yangu alikuwa na timu ya kandanda,mikaka ile ya themanini. Na siku mbili hivi kabla ya mechi ya kuchubuana,wachezaji walikuwa wanapiga kambi nyumbani kwetu. Wale kushiba shibe yao na kama ada ya sheria kujipasha moto misuli.''
Kama tujuavyo mwacha mila ni.mtumwa. katika ulimwengu wa mpira,kuwa sako kwa bako  na  vidosho kabla ya mechi kulikuwa nuksi ya mbwa kutia guu msikitini. Kulikuwa chira hatari ajabu! Kitendo hicho kilidaiwa kwa madai kwamba kinasababisha timu kuchabangwa ovyo mabao nusura kubaki hoi. Vikosi vingi ya timu nyingi tu viliyoa na kudokeza bayana kuwa tabia hiyo kati ya wachezaji wao ilichanga bia kudunda na kushindwa  miguu juu vichwa chini! Ama kweli tabia ni kia la mwili. Sijakosea katu.
   Wanawake( kina Hawa)/walikuwa mwiko kuwakaribia seuze kuwa bega kwa bega nao wanaume kabla ya  mchuano halisi ili timu iweze kufaulu vyema.
    Kwa wanasoka maarufu sawa na dhahabu,kutuhumiwa kwa ubakaji na kuingiliana na mabinti kwenye madanguro ya mighahawa- imebakia na kusalia kuwa paka mweusi kizani.
  Ni dhahiri shahiri kama utofauti wa mamba na kenge kwamba,wachezaji hawa sena wapo kati kwa kati. Wanaweza kupoteza umilisi wa taaluma yao katika michezo. Hata majina yao yanaweza kazama chubwi kuzimuni kwa dakika chache tu. Kisa tuhuma za ubakaji. Chanzo  kikiwa kashifa hizi zisizo na sifa bali hatari chungu.
   Kashifa kama hizi humfanya mchezaji kuhahirishwa na kunyimwa ushiriki kwenye michezo na FIFIA pamwe na mashirika mengine ya mpira.
   Shimo la kimo shabiku ya vinywa vyao ngwena hujitokeza pia. Wafadhili waliowawekezea wachezaji hawa,huwenda wakajiondoa na kujitenga sawa ardhi na mbingu. Hali itakuwa si hali tena.
    Ajabia ya Musa,kishangao kwa.Farao. Mambo hayo ni tofauti.mno barani Afrika. Eti totoshoo limtuhumu mchezaji kwa.ubakaji! Masikini yeye!Hakuna ripota wala.mwanahabari atakaye mtegea sikio la huruma ndi! Hamna gazeti maarufu au pengine lile hivi hivi linaweza kujitolea.mhanga kuisikiliza tuhuma wala  kuzamia kilio cha kite chake binti kama huyu. Dunia rangi rangile.
   Hivyo,si choza wala siri kudai kuwa michezo na 'mahaba' yana uhusiano japo tengetenge au tata. Lakini,wachezaji wote,mabezo kando wanafaa kujibari mashakafundo kama haya ili kuweka ngao safi kwenye ndoto zao za uchezaji.
   Mathslani,Wanaspoti matajri ni nadra mno kwao kujipatia jiko au kufunga nikahi kutokana na mahusiano ya kuyumbayumba kati yao na wandani mbalimbali. Ndivyo huwa kwamba wachezaji kama hawa hawana misingi dhabiti ya kudhihirisha wapenzi wao ni kina nani haswa.
   Wachezaji hawa bila shaka wana satua ya kubwaga kando(kwenye kaburi la sahau) mashaua ya kiburi chao ili waoneshe heshima kuu kwa wanawake walio binadamu mfano sawa nao wenyewe.
Makala yameandikwa na :Msheshe.Rashid
Mwalimu;Mary Immaculate complex Nairobi.

Comments

Popular posts from this blog

NI SABABU ZIPI ZINAZOFANYA MZUNGUMZAJI WA LUGHA KUFANYA MAKOSA YA KISARUFI NA KIMATAMSHI NA KIMANTIKI KATIKA LUGHA?

Methali, Vitendawili, nahau, misemo,

NADHARIA ZINAZOELEZEA CHIMBUKO LA FASIHI SIMULIZI/MASIMULIZI