MFUMO WA CBC KUMFAIDI BARAKA JEFFA PAKUBWA.

MFUMO WA CBC KUMFAIDI BARAKA JEFFA PAKUBWA.
Baraka Jeffa ni mtoto wa tatu kati ya wana wanne. Analelewa katika familia ya mvyele mmoja ambaye ni mama. Hatima ya babake bado ni taharuki. Anasoma katika Shule ya Msingi ya Ronald Ngala iliyo katika Eneo Gatuzi la Mombasa,mtaa wa Sparki. Ni mzawa wa kijiji cha Majengo ya Simba kitongoji cha Swale Nguru.
 
Ghulamu huyu yu katika darasa la nne na tangu akiwa darasa la kwanza,amekuwa na hulka ya kumdadisi mamake akishona nguo. Sasa hivi kazi hii ya ushonaji ameitwaa na kuijua kama kiganja chake cha mkono. Baraka amekubuhu katika kazi hii ya ushonaji kwani sasa anawajibika kwa kuwauni nduguze kwa kuwashonea na kurekebisha nguo zao kwa kutia viraka. Isitoshe, yeye hujirebishia sare yako ikiwa na hitilafu. Ana mazoea ya kutafuta viraka vikuukuu  kwa majirani na hata kwa wanaofanya kazi hii adimu. Anapofanikiwa kupata viraka hivyo,yeye huviunganisha na kuunda zulia pazia ama kifaa cha kupiga deki.
Mbali na kushona mtoto huyu hujihusisha na masuala ya kandanda ijapokuwa kazi yake ya kushona anaienzi kama mboni ya jicho. Licha ya kuwa Baraka anaienzi kazi hii,kuna changamoto ainati ambazo yeye hupitia. Kwanza ni mahali anaposhonea kuwa padogo mno na ndipo jikoni na kubwa ni kuwa hakuna umeme. Mamake hampatii fursa na situa kubwa ya kufanisha kazi yake kwani naye pia huhitaji kushona ikumbukwe kuwa ndiyo kazi inayomletea mapato. Mwisho yeye ni mwanafunzi na hana saa ya kushona kwani aghalabu hujisabilia kukamilisha kazi mradi ya walimu mwanzo ndiyo arejelee kazi hii ya ushonaji.
Baraka Jeffa angenda dua lake limfikie mhisani mmoja ili amuauni kwa kumnunulia cherehani na mengineo ndiyo ndoto yake ya kuwa mshonaji wa kupigiwa mfano itimie.
.
Baraka Jeffa ni mtoto wa tatu kati ya wana wanne. Analelewa katika familia ya mvyele mmoja ambaye ni mama. Hatima ya babake bado ni taharuki. Anasoma katika Shule ya Msingi ya Ronald Ngala iliyo katika Eneo Gatuzi la Mombasa,mtaa wa Sparki. Ni mzawa wa kijiji cha Majengo ya Simba kitongoji cha Swale Nguru.
Ghulamu huyu yu katika darasa la nne na tangu akiwa darasa la kwanza,amekuwa na hulka ya kumdadisi mamake akishona nguo. Sasa hivi, kazi hii ya ushonaji ameitwaa na kuijua kama kiganja chake cha mkono. Baraka amekubuhu katika kazi hii ya ushonaji kwani sasa anawajibika kwa kuwauni nduguze kwa kuwashonea na kuwarekebishia nguo zao kwa kutia viraka. Isitoshe, yeye hujirekebishia sare yake ikiwa na hitilafu. Ana mazoea ya kutafuta viraka vikuukuu  kwa majirani na hata kwa wanaofanya kazi hii adimu. Anapofanikiwa kupata viraka hivyo,yeye huviunganisha na kuunda zulia, pazia ama kifaa cha kupiga deki.
Mbali na kushona mtoto huyu hujihusisha na masuala ya kandanda ijapokuwa kazi yake ya kushona anaienzi kama mboni ya jicho. Licha ya kuwa Baraka anaienzi kazi hii,kuna changamoto ainati ambazo yeye hupitia. Kwanza ni mahali anaposhonea kuwa padogo mno na ndipo jikoni na kubwa ni kuwa hakuna umeme. Mamake hampatii fursa na situa kubwa ya kufanisha kazi yake kwani naye pia huhitaji kushona ikumbukwe kuwa ndiyo kazi inayomletea mapato. Mwisho yeye ni mwanafunzi na hana saa ya kushona kwani aghalabu hujisabilia kukamilisha kazi mradi ya walimu mwanzo ndiyo arejelee kazi hii ya ushonaji.
Baraka Jeffa angependa dua lake limfikie mhisani mmoja ili amuauni kwa kumnunulia cherehani na mengineo ndiyo ndoto yake ya kuwa mshonaji wa kupigiwa mfano itimie.

Comments

Popular posts from this blog

NI SABABU ZIPI ZINAZOFANYA MZUNGUMZAJI WA LUGHA KUFANYA MAKOSA YA KISARUFI NA KIMATAMSHI NA KIMANTIKI KATIKA LUGHA?

Methali, Vitendawili, nahau, misemo,

NADHARIA ZINAZOELEZEA CHIMBUKO LA FASIHI SIMULIZI/MASIMULIZI